30 Juni 2025 - 23:55
Muharram 1447H | Falsafa ya Maombolezo na Kumbukumbu ya A'shura - 1 + Video

Kuipenda Haki na Kuitetea Haki, Kuupenda Ukweli na kuutetea Ukweli, Kuupenda Uadilifu na Kuitetea Uadilifu, kuwa pamoja na Haki, ukweli na uadilifu ... Yote hayo ni sehemu ya Malengo adhimu ya Harakati ya Imam Hussein (as), yenye kutoa matunda yake mazuri kwa kila zama.

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika Mwezi wa Muharram - Tunakumbuka Mauaji dhidi ya Imam Hussein (as) - Mjukuu wa Mtume wetu Muhammad (saww) na kuhuisha mafunzo yote mazuri yaliyomo ndani ya Harakati ya Mapinduzi ya Imam Hussein (as) kama vile:

1_Kuipenda Haki na Kuitetea Haki.

2_Kuupenda Ukweli na kuutetea Ukweli.

3_Kuupenda Uadilifu na Kuitetea Uadilifu.

4_Kuwa pamoja na Haki, Ukweli na Uadilifu.

Yote hayo ni sehemu ya Malengo adhimu ya Harakati ya Imam Hussein (as), yenye kutoa matunda yake mazuri kwa kila zama.

-

Qasim Bin Hassan (as) Namna Alivyopambana Kuitetea Haki, Ukweli na Uadilifu Katika Vita vya Karbala

Katika vita vya Karbala walikuwepo Vijana waliosimama kwa Msimamo thabiti, kuutetea Uislamu na Mafundisho ya Uislamu - waliojitokeza kukabiliana na adui wa Uislamu halisi wa Mtume Muhammad (saww). Vijana hao ni pamoja na kijana huyu anayeitwa: Qasim bin Hassan bin Ali bin Abi Talib (Amani iwe juu yao). Kwa hakika alikuwa kijana Shujaa katika kuitetea Haki, kuutetea Ukweli, na Kuutetea Uadilifu. 

Muharram 1447H | Falsafa ya Maombolezo na Kumbukumbu ya A'shura - 1 + Video

Your Comment

You are replying to: .
captcha